Bongo Fc


Morocco mabingwa chan

Timu ya Morocco imetwaa ubingwa wa mashindano ya Kombe la CHAN, baada ya kuichapa Nigeria mabao 4-0, katika mchezo wa fainali.

Morocco inakuwa timu ya kwanza kuwa mwenyeji wa mashindano hayo yanayoshirikisha wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kutwaa ubingwa.

Timu hiyo ilipata ushindi mnono baada ya Nigeria kucheza pungufu ikiwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya Peter Eneji kulimwa kadi nyekundu.

Mabao ya Morocco katika mchezo huo yalifungwa na Zakaria Hadraf, Walid El Karti na Ayoub El Kaabi, aliyefunga mawili.

Mshambuliaji El Kaabi alichaguliwa mchezaji bora wa mashindano hayo. Nyota huyo amefikisha mabao tisa katika mashiandano hayo mwaka huu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.