Bongo Fc


Ronaldo aweka rehani kibarua cha zidane madrid

Mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo, ameshindwa kutuliza presha ya bosi wake Zinedine Zidane. Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno, ndiye mfungaji bora wa Real Madrid katika mashindano mbalimbali.

Ronaldo, kinara wa kufunga mabao katika kikosi cha Real Madrid amegonga mwamba kuokoa kibarua cha Zidane. Zidane amekalia kuti kavu baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri tangu kuanza msimu huu.

Real Madrid imeshindwa kufua dau mbele ya watani wake wa jadi Barcelona ambayo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania. Wakati Barcelona ikiwa kileleni kwa pointi 57, Real Madrid inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 39.

Jinamizi la matokeo mabaya limeendelea kuitesa Real Madrid, baada ya juzi usiku kuporwa tonge mdomoni dhidi ya Levante. Zidane akiwa na matumaini ya kushusha presha katika mchezo huo, aliduwazwa dakika moja kabla ya mpira kumalizika kwa bao la kusawazisha.

Giampaolo Pazzini alipeleka kilio kwa Zidane kwa kufunga bao dakika moja kabla ya mpira kumalizika. Real Madrid ilikuwa inaongoza mchezo huo hadi dakika ya 88 kabla ya Pazzini kufunga bao dakika ya 89.

Zidane, nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa, aliondoka uwanjani akiwa amefura kwa hasira. “Tulimiliki mpira vizuri hasa kipindi cha kwanza, lakini baada ya kufunga bao la pili hali ilikuwa tofauti, tulishindwa kujilinda kuepuka wapinzani wetu kusawazisha,” alisema Zidane.

Kocha huyo alisema mpira una njia zake, wamefanya makosa yaliyoigharimu timu katika mchezo aliodai walikuwa na nafasi kubwa ya kupata pointi tatu muhimu kwenye Ligi Kuu Hispania.

Licha ya kuwa na tofauti ya pointi 18 dhidi ya Barcelona, lakini hawezi kurusha taulo katika kampeni ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Hispania.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.