Bongo Fc


Conte amgeuzia kibao abramovich, ataka mambo hadharani

Kocha wa timu ya Chelsea, Antonio Conte, anataka kura ya umma ya kuaminika kutoka kwa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich, ili kukomesha hali ya kutokuwa na uhakika wa nafasi yake.

Kocha huyo wa Chelsea ambaye anakerwa na sera ya usajili ya klabu hiyo, anaelezwa kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wake.

Abramovich, ambaye yupo jijini London wiki hii, amekuwa na rekodi ya kufukuza makocha watano ndani ya nusu msimu. Conte alisema, “Natakiwa kuwa mkweli, wakati kuna minong’ono kama hii au tuhuma baada ya mchezo wa kwanza wa msimu dhidi ya Burnley, ningependa klabu iandae taarifa rasmi ya kwamba inaniamini katika kazi yangu.

“Lakini kwa kweli nahitaji maelezo ya kupinga tuhuma hizi, changamoto ni kwamba hapakuwa na jambo hili kabla. Ni jambo kubwa kubadili mtazamo uliokuwa sasa, ila kuna mtu mmoja ambaye anaweza kuzungumza na kubadili kila kitu.”

Chelsea iliwahi kutoa taarifa kwa umma Oktoba 2015 ikiwa chini ya Jose Mourinho, ambaye alitimuliwa baada ya miezi miwili wakati huo akiwa ameongeza mkataba wa miaka minne Agosti baada ya kushinda taji la Ligi Kuu England.

Conte alidai kwamba, anataka kuwa mkweli, kwa kuhitaji mkataba wake usitishwe na kuongeza kwamba: “Tumefanya kazi kubwa katika hii klabu. “Kama klabu itakuwa imeelewa jambo hili na inataka kuniongezea mkataba mpya, tunaweza kuzungumza.

“Kwanini isiwe hivyo? Matamanio na utayari wangu ni kuendelea kufanya kazi katika klabu hii.”

Conte ameshuhudia Manchester City ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Aymeric Laporte, kuliko wachezaji watatu waliosajiliwa na Chelsea katika usajili wa Januari mwaka huu.

“Kama unajilinganisha na mambo ya nyuma, hali imebadilika sana,” alisema Conte na kuongeza: “Unatakiwa kuelewa hilo baada ya kazi kubwa. “Nafikiri klabu kama Chelsea inatakiwa kuwa na subira kuliko timu nyingine. “Kujaribu kufanya kazi kwa pamoja na wachezaji unatakiwa kuwa na subira. Msimu uliopita tulifanya jambo kubwa sana, lakini msimu huu hatuko sawa.”


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.