Bongo Fc


Rooney amkubali guardiola, aiponda manchester united

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amesema klabu hiyo haina ubavu wa kuipiku Manchester City msimu ujao.

Rooney ametoa kauli hiyo alipokuwa mgeni katika kituo cha televisheni Sky Sports wakati akihojiwa na mchambuzi Jamie Carragher.

Rooney alisema Man City ni timu imara ni vigumu Man United kuisimamisha katika mechi za msimu ujao.

Nguli huyo mwenye miaka 32, alisema Man United inatakiwa kufanya kazi ya ziada kuwanyamazisha majirani zao.

Rooney alisema Man City imekuwa kwenye kiwango bora kwa kuwa inatumia mfumo wa Barcelona.

Kocha Pep Guardiola alikuwa nahodha wa Barcelona kabla ya kuwa kocha aliyeipa mafanikio.

“Hawawezi kuwapiku msimu huu. Lazima niwe mkweli hata msimu ujao itakuwa ngumu sana kuwapiku. Hata kama siyo jambo jema kusma, lakini ukweli navutiwa na Man City,” alisema Rooney aliyewahi kuwa nahodha wa England.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.