Bongo Fc


Kwa hili! ramsey kuwafuata ozil, aubameyang

Klabu ya Arsenal kwa mara ya kwanza inapitia kipindi kigumu kuhusu mishahara ya wachezaji. Kocha Arsene Wenger alifumba macho na kutoa pauni 350,000 kwa mchezaji wa kiungo Mesut Ozil.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, alimtikisa muda mrefu Wenger, baada ya kugoma kutia saini mkataba mpya. Baada ya malumbano ya muda mrefu na kuhofia kumpoteza, Wenger aliamua kutoa donge nono la mshahara kwa Mjerumani huyo.

Mbali na Ozil, Arsenal imetoa mshahara mnono kwa Pierre-Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitryan, ambao kila mmoja anakaribia kuvuna mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.

Baada ya kumalizana na kina Ozil, Arsenal inaweza kuingia katika mzozo mwingine kwa mchezaji Aaron Ramsey. Ramsey amekuwa nyota Arsenal baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa Ligi Kuu England walioshinda mabao Arsenal’s 5-1 dhidi ya Everton.

Mchezaji huyo anaweza kuibua mjadala na Wenger kuhusu mkataba mpya baada ya kubakiza miezi 18 kabla ya kumalizika. Hata hivyo, hakuna mazungumzo baina ya pande hizo kuhusu mkataba mpya. Ramsey analipwa mshahara pauni 110,000 kwa wiki.

Arsenal italazimika kumwangukia Ramsey kutia saini mkataba mpya kwa kuwa haina uhakika na ubora wa Danny Welbeck, aliyebakiza miezi 18 kumaliza mkataba.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.