Bongo Fc


Ukisikia okwiiiiiiiiii, simba kacheka

Okwiii! Hivyo ndivyo ilivyosikika kutoka kwa mashabiki wa Simba waliofurika Uwanja wa Taifa jana baada ya kumshuhudia mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi akifunga bao pekee wakati wakiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC.

Bao hilo limemwezesha Okwi kuendelea kukaa kileleni mwa orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu akifikisha mabao 13, matatu mbele ya Obrey Chirwa wa Yanga ambaye anamzidi John Bocco 'Adebayor' wa Simba kwa bao moja.

Kadhalika, ushindi huo umeifanya Simba kuendelea kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 41 ikifuatwa na Yanga wenye pointi 34 wakati Azam FC wenyewe wamebakia na pointi zao 33.

Bao hilo la Okwi lilipatikana katika dakika ya 36 baada ya kazi nzuri iliyoanzia kwa beki Erasto Nyoni kisha kwa Asante Kwasi aliyemimina krosi iliyomkuta mfungaji huyo anayeongoza kwenye ligi msimu huu.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, sasa itaelekeza maandalizi yake katika kuiwinda Gendarmerie ya Djibout kwenye mechi ya awali ya Kombe la Shrikisho Afrika itakayopigwa Uwanja wa Taifa Jumapili.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.