Bongo Fc


Sanchez ndani ya hukumu nzito, jela miezi 16 baada ya kukwepa kodi

Hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili mshambuliaji mpya wa Manchester United Alexis Sanchez imetoka hii leo na mshambuliaji huyo kuhukumiwa miezi 16 jela.

Sanchez alikuwa akikabiliwa na kesi ya ukwepaji kodi wakati alipokuwa nchini Hispania na mamlaka za kodi nchini humo zinadai Alexis alikwepa takribani £900,000.

Lakini kwa sheria za nchini Hispania Alexis Sanchez hatakwenda jela kwa kuwa hukumu yake haizidi miaka miwili na pia hii ni mara ya kwanza kwake kupewa hukumu ya namna hiyo.

Lakini mshambuliaji huyo atalazimika kulipa faini ya kiasi cha £525,000 kutokana na kosa hilo ambalo alilifanya katika miaka yake mitatu aliyokuwa akiitumikia Barcelona.

Hukumu ya Sanchez inakuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanga uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho ambaye naye anatajwa kufanya kosa kama hilo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.