Bongo Fc


Wenger awavuruga jose mourinho, pep guardiola

Ghafla tu Arsene Wenger amepindua meza. Amewageuzia sura makocha wenzake, Pep Guardiola na Jose Mourinho ambao muda wote walimwona kuwa ni mnyonge.

Kwenye dirisha lililopita la usajili wa wachezaji, Guardiola na Mourinho walikuwa wakimtishia Wenger kumpora mastaa wake, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Kumbuka mastaa hao mikataba yao ilikuwa inaelekea ukingoni na ingefika tamati mwisho wa msimu huu na baada ya kufahamu kwamba Wenger alikuwa anasuasua kuwapata mishahara wanayotaka ili wakali hao wabaki Emirates, Mourinho na Guardiola wakaja na ahadi nyingi za kuwalipa mishahara minono mastaa hao ili tu waende kwenye timu zao huko Manchester United na Manchester City.

Wenger akakubali kushindwa kwa kumwaachia Sanchez, ambaye alipiganiwa na Guardiola na Mourinho. Mourinho akashinda na hadi unasoma habari hii, Sanchez ni mchezaji wa Man United na ameshafunga bao moja kwenye Ligi Kuu England.

Baada ya kukamilisha dili la Sanchez, Mourinho na Guardiola walikuwa wakijipanga kumvamia tena Wenger mwishoni mwa msimu kwenda kuchukua silaha yake iliyobaki, yani Ozil.

Lakini, ghafla, Wenger amebadilika na yeye kuanza kutumia silaha ya pesa kama wanavyotumia wapinzani wake hao. Akampa Ozil mkataba mpya wa miaka mitatu na mshahara mzito wa Pauni 300,000 kwa wiki.

Kwa maana hiyo, Arsenal imekuwa si timu ya wanyonge tena. Mshahara ambao wanamlipa Ozil, unamfanya kuwa mchezaji namba mbili anayelipwa vizuri zaidi kwenye Ligi Kuu England. Sanchez wa Man United ndiye anayeongoza, akilipwa Pauni 350,000 kwa wiki kwenye mshahara wake.

Lakini, Wenger akaonyesha tena jeuri ya pesa kwa kuwapa mishahara mikubwa Henrikh Mkhitaryan na straika wake mpya Pierre-Emerick Aubameyang.

Mastaa wote hao Wenger anawalipa vizuri, hivyo hawezi kutetemeshwa tena na Guardiola na Mourinho ambao muda mrefu walikuwa wakitumia pesa zao kumnyanyasa.

Mkhitaryan na Aubameyang kila mmoja anapokea mshahara unaoanzia Pauni 180,000 kwa wiki. Huko Man City kwa Guardiola, mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ni Kevin de Bruyne, anayedaiwa kulipwa Pauni 2800,000 kwa wiki.

Kabla ya hapo, Wenger alikuwa akiwalipa kiduchu sana mastaa wake, ambapo wakati huo Ozil alikuwa akipokea Pauni 1400,000 tu kwa wiki. Alikuwa akidiwa hata na kipa David De Gea (Pauni 200,000 kwa wiki), alikuwa akikaribiwa kabisa na Jesse Lingard (Pauni 100,000).

Sasa Wenger ameamua kuamsha makubwa yake kwenye matumizi ya pesa na ripoti zinadai kwamba msimu wa msimu kwenye dirisha la usajili atashusha mashine za maana, ambazo ataweza kuzituliza tu kwa kuzilipa mishahara ya maana.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.