Bongo Fc


Kwasi, mghana aliyeifunga simba mara ya mwisho, hadi leo haijafungwa tena..

Huku Simba ikiwa ndiyo kinara katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa pointi 41 bila kupoteza mchezo hata mmoja, beki wa timu hiyo, Mghana Asante Kwasi ndiye mchezaji wa mwisho kuifunga timu yake ya sasa akiwa Lipuli FC.Simba imefanikiwa kucheza michezo 17 mpaka sasa bila kupoteza mchezo wowote na ikiruhusu mabao sita ikiwa ni timu pekee ambayo imefungwa mabao machache kuliko timu zote.

Mara ya mwisho Simba kuruhusu bao ilikuwa ni Novemba, 26, mwaka 2017 ilipocheza na Lipuli FC katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo walitoa sare ya bao 1-1 bao la wapinzani likiwa la Kwasi ambaye sasa yuko Simba.

Baada ya hapo, Simba imecheza michezo takribani sita bila kuruhusu bao hata moja ambapo imecheza dhidi ya Ndanda FC (2-0), Singida United (4-0), Kagera Sugar (0-2), Majimaji (4-0), Ruvu Shooting (3-0) na juzi dhidi ya Azam FC (1-0).


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.