Bongo Fc


Wenger adai wachezaji wa uingereza ni 'mabingwa' wa kujiangusha uwanjani

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amelalamika kwamba wachezaji wa Uingereza wamekuwa na tabia ya kujirusha na kutengeneza adhabu, chombo cha habari cha BBC Sports kimeripoti.

Amesema mchezaji wa Tottenham Dele Alli alifanya kitendo hicho kwenye mchezo wa jumapili huko Liverpool na kusababisha mwamuzi kutoa adhabu ya penalti.

Mchezaji mwingine ambaye anatuhumiwa kufanya kitendo hicho ni Harry Kane, alifanya hivyo kwa mchezaji Virgil van Dijk wa Liverpool na kusababisha mpira wa adhabu.

Wenger amesisitiza kwamba anakumbuka kumekuwa na kesi za wachezaji kutoka nje ya Uingereza, lakini wachezaji wa Uingereza sasa wameiga tabia hiyo na wamekuwa vinara wa matukio hayo kuliko wachezaji wengine.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.