Bongo Fc


Spurs yaishushia kipigo arsenal

Klabu ya soka ya Arsenal imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzani wao jijini London Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza hapo jana.

Katika mchezo huo ambao umepigwa kwenye uwanja wa Wembley ambao ni nyumbani kwa Tottenham bao pekee la timu hiyo limefungwa na mshambuliaji Harry Kane dakika ya 49.

Aidha, matokeo hayo yanaifanya Arsenal kuendelea kubakia katika nafasi ya sita ikiwa na alama 46 kwenye mechi 27 za ligi, huku Tottenham wakiendelea kukaa katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 52 baada ya mechi 27.

Katika mchezo wa jana, Arsenal imewachezesha wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye dirisha dogo ambao ni Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang lakini wameshindwa kuisadia timu hiyo kupata ushindi.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.