Bongo Fc


Simba kama kawaida yao, yaanza na 4g kombe la shirikisho afrika

Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendermarie mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumapili.

Mabao ya Simba yalifungwa na Said Ndemla, John Bocco (2) na Emmanuel Okwi ambaye alifunga karamu ya mabao.

Ushindi huo unawapa nafasi Simba kusonga mbele kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho ambapo mchezo wa marudiano wapinzani wao watahitajika kushinda mabao 5-0.

Nyota ya Simba inayong’ara kwwenye mechi za Ligi Kuu imeakisi pia kwenye mashindano hayo ya kimataifa ambao wamefanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.