Bongo Fc


Kwa mwendo wa kwasi, zimbwe analazimika kufanya kazi ya ziada simba

Inaonekana kuwa beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein Zimbwe analazimika kukaza buti hasa, la sivyo, First Evelen atakuwa akiisikia tu radioni.

Hii inatokana na beki Mghana, Asante Kwasi ambaye Simba ilimsajili kama beki wa kati kuonyesha uwezo mkubwa akicheza pembeni kushoto. Kwasi amekuwa chachu ya mabao mengi ya Simba huku akionyesha uwezo mkubwa wakati wa kulinda na kushambulia.

Krosi zake nyingi zimekuwa tegemeo la kusababisha mabao ya Simba au kutengeneza mashambulizi bora. Hii inamfanya Zimbwe ambaye alikuwa “mwenye namba” msimu uliopita kuwa katika wakati mgumu sana.

Zimbwe ameendelea kubaki benchi na chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Mfaransa, Pierre Lechantre na msaidizi wake Mrundi, Masoud Djuma kuwa ni Kwasi na kama ataendelea kuwa fiti basi Zimbwe lazima afanye kazi hasa.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.