Bongo Fc


Psg yamtia hofu ronaldo

Mshambulaiji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameonesha kuihofia PSG kuelekea katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa leo katika dimba la Santiago Bernabeu nchini Hispania.

Ronaldo amekiri kwamba PSG ina wachezaji wazuri na wanaoifanya kuwa bora kwa sasa, hivyo ili timu yake ipate ushindi inahitaji kuwa kwenye ubora zaidi.

Hata hivyo, nyota huyo wa Ureno, amesema wataonesha kuwa Real Madrid ni timu imara na yenye uzoefu mkubwa, na kwamba watacheza kwa nguvu kwenye mechi zote mbili dhidi ya matajiri hao wa Ufaransa na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Ronaldo anayasema hayo baada ya wikiendi iliyopita kufunga ‘hat-trick’ yake ya kwanza kwenye La Liga msimu huu, Real Madrid ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Real Sociedad kwenye dimba la Saintiago Bernabeu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.